AUCHO, MAYELE KUWAKOSA TAIFA JANG’OMBE MAPINZUZI LEO

MASTAA wa Yanga, Khalidi Aucho na Fiston Mayele, hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe na kwamba wataunguruma dhidi ya KMKM kesho kutwa Ijumaa.

Aucho ameshindwa kusafiri na kikosi hicho kufuatia kuomba ruhusa ya kwenda kwao Uganda kwa ajili ya kuiona familia yake, huku Fiston Mayele naye yupo nchini DR Congo, kwa ajili ya kuhani msiba wa shemeji yake na anatarajiwa kuungana na timu mapema Alhamisi.

Chanzo chetu kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatano kwamba, Aucho na Mayele wameshindwa kuambatana na timu iliyoondoka jana jioni kwa kuwa wote wamesafiri kwenda makwao hivyo wanatarajia kuungana na kikosi mapema Alhamisi ya Januari 6, mwaka huu.

“Aucho sio sehemu ya msafara pamoja na Mayele kwa kuwa wote wapo makwao, hivyo tunatarajia watakuwa nasi katika mchezo dhidi ya KMKM unaotarajiwa kupigwa Januari 7, mwaka huu, hivyo nina imani kutokana
na ratiba zao zilivyo watawahi na huenda wakawa sehemu ya mchezo wetu siku hiyo,” kilisema chanzo hicho.

Yanga wanakwenda kushiriki michuano hiyo wakiwa mabingwa watetezi wakiifunga Simba kwenye
fainali ya mwaka jana kwa penalti 4-3 baada ya kutoka suluhu.

Yanga wenyewe tayari wametambulisha wachezaji wapya watatu ambao ni Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC, Denis Nkane (Biashara United) na Abdoultwalib Mshery (Mtibwa Sugar). Bwalya aliyewahi kuichezea Al Ahly ya nchini Misri, hivi karibuni alitangaza kuvunja mkataba na timu ya
Yeni Malatyaspor baada ya kutolipwa mshahara kwa miezi minne.