Home Sports KABWILI AVUNJA UKIMYA YANGA

KABWILI AVUNJA UKIMYA YANGA

PAMOJA na kuwepo na tetesi nyingi za kuachwa pale Yanga, kipa chaguo la pili Ramadhani Kabwili, amevunja ukimya kwa kusema yeye bado ni mali ya Wanajangwani hao na kwamba ameomba tu mapumziko kwa muda kisha atarudi kukiwasha kikosini hapo.

Kabwili aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2016/17 akiwa kinda kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa na Kocha Hans van Der Pluijm kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo, aliwika akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U 17, Serengeti Boys iliyokwenda kushiriki AFCON mwaka 2017 hukoGabon.

Takribani mwezi sasa uongozi wa Yanga umekaa kimya juu ya habari za Kabwili kutokuwa ndani ya kikosi hicho jambo ambalo limezidi kuleta mkanganyiko kwa wadau wa soka na hata uongozi unapoulizwa juu ya uwepo wake ndani ya timu umekuwa hauna jibu la kuridhisha zaidi ya kusema ameomba kupumzika.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kabwili amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa tetesi za kuachwa na Yanga, yeye hana taarifa hiyo zaidi anachokijua ni kwamba aliomba muda wa kupumzika kama mchezaji halali wa timu hiyo, hivyo hana mpango wowote wa kwenda timu nyingine na muda wowote ataungana na wenzake kikosini.

“Ninachokijua mimi bado ni mchezaji wa Yanga, hivyo sina mpango wa kusajiliwa kwingine, zaidi nimeombamapumziko ya muda na siku yoyote kuanzia sasa nitaungana na timu, popote itakapokuwa, haijalishi sijaendaMapinduzi Cup,” alisema Kabwili.

Previous articleAUCHO, MAYELE KUWAKOSA TAIFA JANG’OMBE MAPINZUZI LEO
Next articleYANGA YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA KILINET NA N-CARDS