Home Sports YACOUBA AANZA MAZOEZI YANGA

YACOUBA AANZA MAZOEZI YANGA

NI habari njema kwa mashabiki wa Yanga baada ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne raia wa Burkina Faso kuanza mazoezi mepesi, huku akitarajiwa kurejea rasmi uwanjani baada ya mwezi mmoja kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote.


Yacouba alipata majeraha ya goti 
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Novemba 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na Yanga kushinda 3-1.

Baada ya kuumia, Novemba 10, mwaka huu Yacouba alipelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu akiongozana na Dokta wa Viungo wa Yanga, Youssef Mohamed, huku taarifa za awali kutoka kwa daktari zikieleza atakaa nje kwa muda wa zaidi ya miezi minne.


Akizungumza na Spoti Xtra, Dokta 
Youssef, alisema: “Kila kitu kipo sawa, kuhusu hali ya Yacouba kwa sasa anaendelea vizuri.


“Ameanza mazoezi mepesi ya peke 
yake ambapo tunatarajia baada ya mwezi mmoja ataanza rasmi mazoezi na timu.”

Previous articleAZAM FC KUIBUKIA ZANZIBAR, KOMBE LA MAPINDUZI
Next articleJANUARI 3,MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU