AZAM FC KUIBUKIA ZANZIBAR, KOMBE LA MAPINDUZI

KIKOSI cha Azam FC leo Januari 2,2022 kimeanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Jana Januari Mosi 2022, Azam FC ilifungua mwaka kwa kupoteza pointi tatu mbele ya Simba baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 2-1Azam FC.

Wanaelekea Zanzibar kulisaka taji ambalo lipo mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Azam FC ipo kundi A ikiwa na timu nyingine ambazo ni Namungo FC, Yosso Boys na Meli Nne City.

Miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa Zanzibar ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Nicolas Wadada,Mathias Kigonya, Rodgers Kola na Ismali Kader.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2 2022 ambapo leo Namungo watamenyana na Meli Nne na kazi ya Azam FC itakuwa ni Januari Nne watamenyana na Meli Nne.