Home Sports VIDEO:PABLO HAKUTAKA MANULA AFUNGWE,PENALTI YA BWALYA AIFUNGUKIA

VIDEO:PABLO HAKUTAKA MANULA AFUNGWE,PENALTI YA BWALYA AIFUNGUKIA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa alikuwa anataka kuona wachezaji wake wanapambana na kushinda bila kufungwa lakini haijawa hivyo kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa mwaka 2022 uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo uliochezwa Januari Mosi,2022 kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula alitunguliwa bao moja na Rodgers Kola wa Azam FC huku Simba ikifunga mabao mawili kupitia kwa Sadio Kanoute na Pape Sakho.

Pablo amesema safu ya ulinzi ilikuwa initimiza majukumu yake lakini makosa waliyofanya yamewagharimu wakafungwa hivyo watafanyia kazi kuelekea mechi zijazo na ameweka wazi kwamba suala la mchezaji wake Bwalya kukosa penalti ni jambo ambalo atalifanyia kazi.

Previous articleLUKAKU ANAFIKIRIA KURUDI INTER MILAN
Next articleAZAM FC KUIBUKIA ZANZIBAR, KOMBE LA MAPINDUZI