Home Sports MSHERY ATAMBULISHWA RASMI YANGA

MSHERY ATAMBULISHWA RASMI YANGA

BREAKING: ABOUTWALIB Mshery ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya kuungana na timu hiyo kwa kazi kwa msimu wa 2021/22.

Anaibuka ndani ya Yanga akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar wakati huu wa usajili wa dirisha dogo ambalo limezidi kushika kasi kwa timu za Bongo

Anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa ndani ya Yanga baada ya kuanza na Salum Aboubakhari, ‘Sure Boy’ aliyesajiliwa bure akitokea Azam FC kwa sababu aliomba kuvunjiwa mkataba wake na timu yake ambayo ilikubai kumuachia bila gharama yoyote.

Ni miaka miwili amesaini Mshery kuitumikia Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunissia.

Previous articleISHU YA KIPA MPYA YANGA MENGINE YAIBUKA
Next articleSIMBA YAIVUTIA KASI AZAM FC