Home Sports SIMBA YAIVUTIA KASI AZAM FC

SIMBA YAIVUTIA KASI AZAM FC

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kimeendelea kuivutia kasi Azam FC.

Mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Januari Mosi 2022 na utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu zote mbili wa ushindani kwa mwaka huo mpya.

Leo Desemba 29 kikosi cha Simba kimefanya mazoezi Uwanja wa Bunju Complex ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kwa mujibu wa Pablo Franco amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanatambua kwamba utakuwa ni mgumu na wenye ushindani mkubwa.

“Utakuwa ni mchezo mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo na tunachohitaji ni pointi tatu muhimu hivyo mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye mazoezi ya leo ni pamoja na John Bocco, Meddie Kagere,Mohamed Hussein,Joash Onyango na Kibu Dennis.

Mbali na mazoezi ya uwanjani pia wachezaji wa Simba wana programu ya mazoezi ya GYM kwa ajili ya kujiweka fiti.

Previous articleMSHERY ATAMBULISHWA RASMI YANGA
Next articleVIDEO:BEKI WA YANGA SHOMARI KIBWANA AFUNGUKIA KUHUSU MAJERAHA YAKE