>

PABLO:HATUKUPOTEZA MUDA KWA MKAPA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa walicheza mpira mbele ya Yanga na hawakutumia muda mwingi kupoteza muda kwa kujiangusha ama kulala uwanjani.

Ilikuwa ni dabi ya kwanza kwa Franco, Desemba 11, Uwanja wa Mkapa na aliweza kugawana pointi mojamoja na watani zake wa jadi baada ya dakika 90 ubao  wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-0 Yanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Franco alisema kuwa uwezo wa wachezaji wake ulikuwa mkubwa mwanzo mwisho jambo lililowafanya wacheze mpira bila kupoteza muda.

“Kila mara walikuwa kwenye haraka ya kuanzisha mpira na kucheza katika hilo najivunia nadhani mmeona namna ilivyokuwa hata kwa kipa (Aishi Manula) alikuwa akipata mpira anaanzisha haraka.

“Kwa wachezaji wangu wote ikiwa ni pamoja na Inonga, (Henock), Kapombe, (Shomari) ninawapongeza kwa kazi nzuri ambayo wamefanya na inaonesha kwamba tulikuwa na maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wetu,” alisema Franco.

Alipowasili Tanzania, Franco aliweza kuishuhudia kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya Tanzania ikicheza Uwanja wa Mkapa.