MABINGWA WA KOMBE LA FA SIMBA KAZINI LEO

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Simba leo Desemba 14 wanatarajiwa kushuka Uwanja wa Mkapa kusaka ushindi kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya kombe hilo.

Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya JKT Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo kwa sasa inaitwa Championship.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku na utakuwa mubashara Azam TV.

Simba ni mabingwa watetezi waliweza kutwaa taji hilo msimu wa 2020/21 baada ya kutinga fainali na kushinda mbele ya Yanga, ilikuwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

Bao la ushindi lilifungwa na nyota wao Taddeo Lwanga ambaye alitumia pasi ya kona ya kiungo wao Luis Miquissone ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Al Ahly ya Misri.