Home Sports DODOMA JIJI YASONGA MBELE YAITWANGA PAN AFRICAN 2-0

DODOMA JIJI YASONGA MBELE YAITWANGA PAN AFRICAN 2-0

DODOMA Jiji FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata leo Desemba 14 imeibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho.

Ilikuwa ni raundi ya tatu ambapo wameweza kushinda mabao 2-0 dhidi ya Pan African ambapo dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa ni sare kwa timu zote mbili.

Mchezo huo umechezwa leo Desemba 14, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Cleophace Mkandala  dk ya 85 na Erick Nkosi 90+3 na kufanya isepe na ushindi mazima.

Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa haikuwa mpango wao kupoteza mchezo wa leo.

Previous articleKIKOSI CHA SIMBA KITAKACHAOANZA DHIDI YA JKT TANZANIA
Next articleSIMBA YASHINDA MBELE YA JKT TANZANIA 1-0