Home Sports SIMBA YASHINDA MBELE YA JKT TANZANIA 1-0

SIMBA YASHINDA MBELE YA JKT TANZANIA 1-0

KIBU Dennis, mshambuliaji wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco amefunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Ulikuwa ni mchezo wa raundi ya tatu na ubao wa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ulisoma Simba 1-0 JKT Tanzania.

JKT Tanzania haikuwa na bahati licha kutengeneza nafasi za kutosha katika uwanja jambo lililofanya wapoteze mchezo huo.

Dakika ya 89 Sadio Kanoute alikosa nafasi ya wazi ndani ya 18 kutokana na pigo la kona ya Ibrahim Ajibu.

Previous articleDODOMA JIJI YASONGA MBELE YAITWANGA PAN AFRICAN 2-0
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO