NYOTA wa Azam FC, Prince Dube tayari amerejea kikosi cha kwanza na kuanza kuonyesha makeke yake ndani ya kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.
Kwenye mchezo wake wa kwanza mbele ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alishuhudia timu ya Azam FC ikigawana pointi mojamoja na Kagera Sugar baada ya ubao kusoma Azam FC 0-0 Azam FC.
Mshambuliaji huyo alikuwa nje ya uwanja kwa muda kwa kuwa hakuwa fiti ila kwa sasa tayari ameweza kurejea ndani ya uwanja.
Msimu wa 2021/22 alikuwa ni mfungaji bora ndani ya kikosi cha Azam FC ambapo alitupia mabao 14 na pasi tano za mabao.
Azam FC kwenye msimamo ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza jumla ya mechi nane.