Home Sports YANGA YAWASHUSHA PRESHA MASHABIKI

YANGA YAWASHUSHA PRESHA MASHABIKI

MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha, amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo kuelekea kwenye
mchezo wa Ligi 
Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa leo Jumamosi, Uwanja wa Mkapa huku akiweka bayana wataibuka na pointi tatu.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kariakoo
Dabi ukiwa mchezo wa kwanza 
kukutana kwa msimu huu kwenye ligi.

“Hakuna sababu ya kuwa na presha unajua mchezo wetu wa ligi dhidi ya Simba ni sawa na mechi nyingine ambazo tumecheza.


“Kuelekea katika mchezo wetu 
dhidi ya Simba, tunahitaji kuona tunapata matokeo mazuri ili tuweze
kushikilia ambapo tupo.

“Mashabiki hawapaswi kuwa na presha huu ni mchezo kama ilivyo michezo mingine hivyo ni suala la kusubiri na kuona,”.


“Utakuwa mgumu kulingana na 
ukubwa wa mchezo husika, huu ni mchezo mkubwa kwa Afrika, hivyo
hata sisi viongozi tunauchukulia 
katika ukubwa huo, ndio maana tunatamani kuwa washindi,” alisema SenzoPrevious articleALIYEWATUNGUA YANGA HAYUPO LEO
Next articleKOCHA:SIMBA ITAFUNGWA NA YANGA