Home Sports NTIBANZOKIZA AWATAMANI KWELI SIMBA KWA MKAPA

NTIBANZOKIZA AWATAMANI KWELI SIMBA KWA MKAPA

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ amesema kuwa anatamani kuanza katika mchezo unaofuata dhidi ya Simba huku akiweka wazi kuwa matarajio yake ni kuipa ushindi timu hiyo katika mchezo huo muhimu.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Simba katika mchezo wa ligi kuu unatorajiwa kufanyika leo Desemba 11, mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote kwani kama Yanga itashinda basi itaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 5 huku endapo Simba ikashinda basi itajihakikishia nafasi yakuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 1

Saido amesema kuwa anatamani kuona anapata nafasi ya kuanza katika mchezo dhidi ya Simba ili aweze kuisaidia timu kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ambao ni muhimu kwao.

“Natamani kuona naisaidia timu, natamani kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza lakini mamlaka hayo ni ya mwalimu siku zote, hivyo siwezi kumpangia lakini mwenyewe natamani kuona napata nafasi ya kucheza, naamini nitakuwa na mchango mzuri kwa timu.

“Unajua licha ya kuwa tutapata pointi 3 kama ilivyokuwa michezo mingine lakini kuzipata pointi 3 mbele ya mpinzani wako ni jambo jema, hivyo mengine ambayo yanahusu mchezo wenyewe nadhani waalimu na benchi la ufundi ndio wanahusika zaidi,” amesema kiungo huyo.

Kiungo huyo kwenye mechi saba ambazo Yanga imecheza msimu huu wa 2021/22 ameweza kucheza jumla ya mechi tatu na amefunga mabao mawili kwa mapigo huru.

Alifunga mbele ya Namungo FC kwa mkwaju wa penalti na bao la pili alifunga mbele ya Mbeya Kwanza kwa pigo la faulo.

Previous articlePAMBA SC KUSHUSHA MAJEMBE YA KAZI
Next articleHILI HAPA JESHI LA SIMBA LITAKALOANZA DHIDI YA YANGA