YANGA:SIMBA WEPESI TU

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Yusuph Athuman, amesema kuwa kama watafanikiwa kujitoa kwa moyo wote katika mchezo dhidi ya Simba, basi anaona wakipata ushindi katika mchezo huo.
Yanga kesho Jumamosi wanatarajiwa kupambana na Simba kwenye mchezo wa ligi kuu katika Uwanja wa Mkapa.
 Mshambuliaji huyo amesema kuwa anaiona mechi dhidi ya Simba ikiwa nyepesi kwao kama wachezaji wote watacheza kwa kujituma zaidi ndani ya uwanja, jambo ambalo anaamini watatekeleza.
“Siri kubwa ya ushindi siku zote huwa ni kujituma na kupambana, hivyo kwetu sisi Yanga kama wachezaji wote tutajituma na kupambana kwa nguvu zote basi naamini tutapata ushindi.
“Lakini kama haitakuwa hivyo basi kutakuwa na ugumu, kwetu wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mapambano kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” alisema mshambuliaji huyo.
Chanzo:Championi