SIMBA: KUCHEZA NA YANGA KAMA TIMU YA DARAJA LA KWANZA

KUELEKEA katika mchezo wa Derby ya Kariakoo, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, amefunguka kuwa kwa namna alivyowatazama Yanga, anaamini Simba itaibuka na ushindi wa mapema.

Kesho Desemba 11,2021 Simba itakuwa
mwenyeji wa Yanga, 
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

 Mangungu alisema kwenye mchezo wa kesho timu hiyo
inaingia uwanjani kucheza 
mchezo wa ligi bila hofu kwani hawaitambui Yanga tena kama wapinzani wao hivyo wanaenda kucheza na timu kama zile za daraja la kwanza au la pili tu.

“Tayari maandalizi ya timu yako vyema na kubwa tunashukuru mchezo huu hautakuwa na presha ya aina yoyote kwetu, kwani tayari Yanga ni timu ya kawaida tu kwetu kwa sasa maana tayari hatuwatambui kama wapinzani wetu.”


Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara aliweka wazi kuwa kwa sasa namna timu hiyo inavyocheza kwa kiwango anaamini kwamba mshindani wao ni Azam FC hasa kwa upande wa dabi.

Jambo hilo limewafanya Simba nao kuamua kuiweka kando Yanga kwenye suala la dabi ikiwa ni katika kulipa kisasi kabla ya kuweza kukutana Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu muhimu.

Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Fiston Mayele.

 

Chanzo:Championi