Home International SIMBA HAITAKI KUTESEKA

SIMBA HAITAKI KUTESEKA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hataki kuteseka kwa kupoteza kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Red Arrows ya Zambia ambao ni wa marudio.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi.

Simba inakumbuka kwamba mchezo wa kwanza ilishinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa hivyo inajukumu la kulinda ushindi huo ili kupata nafasi ya kusonga mbele.

Ikiwa nchini Zambia imeendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea kwenye mchezo huo.

Pablo amesema:”Najua utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia kwamba watakuwa nyumbani na uwanja wao mzuri hilo halitupi tabu hatutaki kuteseka kwenye mchezo wetu ama kupoteza.

“Hatutaki kuona kwamba tunasonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho tukiwa tumepoteza, tuna wachezaji wazuri na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu,” amesema.

Ni mabao ya Meddie Kagere aliyefunga bao moja akitumia pasi ya Bernard Morrison katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo kiungo huyo yeye alitupia mabao mawili.

Previous articleDAU LA HAALAND LAFICHWA
Next articleCHELSEA YACHAPWA 3-2 LIGI KUU ENGLAND