MORRISON ATOA NENO BAADA YA KUPATA MILIONI ZAKE

KUNGO mshambuliaji wa Simba Bernard Morrison,amesema kuwa wachezaji wote ambao aliingia nao kwenye fainali ya kuwania tuzo bora kwa mchezaji chaguo la mashabiki walistahili tuzo hiyo lakini mwisho wa siku yeye amechaguiwa kuwa mshindi.

Jana Desemba Pili, Morrison aliweza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Novemba wa Simba.

 

Morrison amekabidhiwa kitita cha Sh 2,000,000 (milioni mbili) kama sehemu ya zawadi kutoka kwa wadhamini wa Klabu hiyo Emirate Aluminium ACP.

Morrison ameshinda tuzo hiyo kutokana na kuwa na kiwango bora katika mwezi huo akichangia kupatikana kwa mabao manne akifunga mawili na kusaidie mengine mawili.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Morrison amewasifu wachezaji alioingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho kuwa kila mtu alistahili kushinda lakini mshindi siku zote ni mmoja hivyo amefurahi kushinda.

 

“Nawapongeza pia nilioingia nao fainali wote tulistahili kushinda lakini mimi nimeibuka kidedea, nimefurahi na hii inanifanya kuendelea kujituma kuisaidia timu,” amesema Morrison.

Wachezaji ambao aliingia nao fainali ni mshambuliaji Meddie Kagere na kiungo Jonas Mkude.

Kuelekea kwenye mchezo wa marudio unaiatarajiwa kuchezwa jumapili, Desemba 5 kikosi cha Simba kinatarajiwa kuibuka nchini Zambia leo Desemba 3 huku Morrison akiwa ni miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa ndani ya kikosi hicho.