Home Sports ISHU YA DUBE NA LYANGA AZAM FC IPO NAMNA HII

ISHU YA DUBE NA LYANGA AZAM FC IPO NAMNA HII

HABARI njema kwa mashabiki wa Azam ni kurejea na kuanza mazoezi kwa mshambuliaji wao Mzimbabwe Prince Dube aliyekosekana kwa muda mrefu, huku chungu nyingine ikiwa ni ile ya kukosekana kwa kiungo mshambuliaji wao Ayoub Lyanga kwa muda wa miezi miwili.

 

Dube amekosekana uwanjani tangu mwezi Mei mwaka huu kutokana na tatizo la tumbo alilolipata kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Rhino Rangers, Lyanga yeye Novemba 16, mwaka huu alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa meno ya juu nchini Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Geita Gold.

Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabith amesema: “Taarifa njema kwa mashabiki wa Azam ni kuwa mshambuliaji wetu Mzimbabwe, Prince Dube anaendelea vizuri na mazoezi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha na hivi karibuni atarejea kwenye majukumu yake uwanjani.

 

“Kuhusiana na Lyanga yeye baada ya kufanyiwa upasuaji Novemba 16, mwaka huu anatarajiwa kukosekana uwanjani kwa kipindi kisichopungua miezi miwili, anaendelea na taratibu za matibabu na hali yake inazidi kuimarika kila siku.”

Jana Novemba 30, Azam FC iliweza kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar na ilishinda bao 1-0 lilipachikwa kimiani na Idris Mbombo kwa pasi ya Bruce Kangwa.

Previous articleGOMES:BANDA ANAHITAJI MUDA NDANI YA SIMBA
Next articleSIMBA V GEITA GOLD, MINZIRO APEWA SOMO,ATHARI KWA SIMBA