Home Sports GOMES:BANDA ANAHITAJI MUDA NDANI YA SIMBA

GOMES:BANDA ANAHITAJI MUDA NDANI YA SIMBA

DIDIER Gomes ambaye aliamua kuondoka ndani ya kikosi cha Simba baada ya kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy Uwanja wa Mkapa amesema kuwa Peter Banda anahitaji muda.

Gomes alikuwa ni Kocha Mkuu wa Simba na mafanikio yake makubwa ni kuipeleka Simba hatua ya robo fainali, alikwama kufanya vizuri kwa msimu wa 2021/22 kwa kuwa timu ya Simba ilitolewa na timu ya Botswana.

Kwa sasa Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco akishirikiana na Seleman Matola na Hitimana Thiery ambao ni wasaidizi.

Banda ni ingizo jipya ndani ya Simba hakuwa katika ubora mbele ya Jwaneng Galaxy kwa kuwa alikosa nafasi mbili za wazi za mabao.

Gomes amesema:”Moja ya wachezaji wazuri ambao wapo ndani ya Simba ni pamoja na Banda lakini anahitaji muda ili aweze kwenda na ile kasi ya kusaka ushindi.

“Unajua ukiwa kijana na unakutana na changamoto mpya katika sehemu tofauti ni lazima kuwe na jambo ambalo litakufanya uone kwamba kuna kitu ambacho hakiendi sawa.

“Kwa wakati ambao nilikuwa namfundisha nilikuwa naongea naye na kumwambia kwamba anahitaji kutulia na kufanya vizuri, basi nina amini kwamba atafanya vizuri lakini anahitaji muda kuwa imara na kutoa kile ambacho wengi wanatarajia,” .

Wakati leo Desemba Mosi timu ya Simba ikiwa na mtihani wa kusaka pointi tatu mbele ya Geita Gold, Banda anapewa nafasi ya kuweza kuanza kikosi cha kwanza.

Previous articleYANGA WAREJEA DAR,KITUO KINACHOFUATA NI DHIDI YA SIMBA
Next articleISHU YA DUBE NA LYANGA AZAM FC IPO NAMNA HII