>

YANGA WAREJEA DAR,KITUO KINACHOFUATA NI DHIDI YA SIMBA

KIKOSI cha Yanga, leo Desemba Mosi,kimerejea Dar kikotea Mbeya ambapo kilikuwa kilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya Kwanza.

Jana, Uwanja wa Sokoine baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mbeya Kwanza 0-2 Yanga.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Fiston Mayele pamoja na Said Ntibanzokiza ambao wamekuwa katika ubora wao.

Kituo kinachofuata kwa vinara hao wa Ligi Kuu Bara inayodhamiwa na NBC ni dhidi ya Simba.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 11 saa 11 jioni.