>

BREAKING:OLE GUNNAR AFUTWA KAZI MANCHESTER UNITED

RASMI leo Novemba 21 Klabu ya Manchester United imethbitisha kuachana na Ole Gunnar Solskjaer ambaye ataondoka ndani ya timu hiyo kwenye majukumu ya kuwa kocha baada ya kushindwa kushinda taji lolote ndani ya miaka mitatu na Michael Carrick atachukua mikoba yake kwa muda kabla ya kocha mpya kuchaguliwa atakayemaliza msimu huu wa 2021/22.

Solskjaer alisaini dili la miaka mitatu lakini anaondoka akiwa hajawa kwenye mwendo mzuri ndani ya kikosi hicho kwa kuwa kwenye mechi tano ameambulia kichapo kwenye mechi zake saba za mwisho ndani ya Manchester United kwenye Ligi Kuu England.

Itakumbukwa kwamba Manchester United ilichapwa mabao 5-0 mbele ya Liverpool wakati akiwa kwenye majukumu kichapo abacho kinatajwa kuwa ilikuwa ni udhalilishaji pia kwenye dabi dhidi ya Manchester City alichapwa mabao 2-0 mwanzoni kabisa mwa Novemba.

Mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni dhidi ya Watford ambapo alishuhudia timu yake ikichapwa mabao 4-1 jambo lililowavuruga mabosi wa United na walikaa naye kikao ili kuweza kujadili hatma yake na taarifa rasmi iliyotolewa na Manchester United imeeleza kuwa kwa sasa hatakuwa ndani ya Manchester United.