Home International SALAH KUIBUKIA LA LIGA

SALAH KUIBUKIA LA LIGA

KLABU ya Barcelona ya nchini Hispania inayoshiriki La Liga imeonesha nia ya kutaka saini ya Mohamed Salah raia wa Misri anayekipiga katika Klabu ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England .

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Hispania, vimesema kocha wa timu hiyo Xavi ameweka wazi nia yake ya kutaka kumsajili Salah kwa gharama yoyote ili atue katika viunga vya Nou Camp.

Salah mwenye miaka 29 amekuwa katika kiwango bora kwa misimu mitatu mfululizo akiisaidia timu yake kushinda taji la Klabu Bingwa Ulaya na taji la Ligi Kuu England.

Barcelona na klabu mbalimbali za soka barani Ulaya zimeonesha nia ya kutaka kunasa saini za nyota huyo wa Liverpool ikiwemo Liverpool wenyewe ambapo mkataba wake unamalizika 2023 na akiwa hajaongeza mkataba mwingine.

Xavi na Barcelona wameweka wazi msimamo wao wa kutokutaka kushindwa kupata saini ya nyota huyo ikiwa kwa sasa wanataka kuijenga upya timu hiyo huku kocha huyo akimtaka Rais Joan Laporte kuhakikisha wanakamilisha usajili huo.

Xavi ni moja ya wachezaji wanaokubali uwezo wa Salah na aliweza kumshuhudia katika Klabu Bingwa ya Dunia mwaka  2019 na kusema  ’Salah ni moja ya wachezaji 10 bora duniani kwa sasa akiwa na uwezo mkubwa sana

Previous articlePABLO AGOMEA BUTUABUTUA NDANI YA SIMBA
Next articleUBORA WA BIDHAA ZA EXPANSE STUDIO KUONEKANA MALTA -2021 STIGMA ULAYA