DANI Alves mwenye miaka 38 ni raia wa Brazil aliwahi kucheza Barcelona msimu wa 2008/16 anaingia kwenye orodha ya nyota waliotwaa mataji mengi akiwa nayo 42.
Lonel Messi raia wa Argentina anakipiga PSG yeye ametwaa mataji 37 ,afanikio yake makubwa aliyapata akiwa ndani ya Klabu ya Barcelona.
Andres Iniesta mwenye miaka 37 nyota aliyekipiga pia ndani ya Barcelona msimu wa 2002/18 pia alicheza na ile timu ya Barcelona B huyu mwamba raia wa Hispania huyu ametwaa makombe 37.
Ryan Giggs mwenye miaka 47maisha yake ya soka ilikuwa ndani ya Manchester United ambapo alicheza jumla ya mechi 672 na kufunga mabao 114 na yeye ni kiungo ametwaa makombe 36.
Kenny Dalglish raia wa Scotland alicheza ndani ya Liverpool msimu wa 1977/90 alicheza jumla ya mechi 355 na kufunga mabao 118 na yeye ni mshambuliaji ametwaa makombe 35.