>

MANCHESTER UNITED KOCHA HUYU ATAJWA

Habari za chini ya kapeti zinamtaja Brendan Rodgers kama kocha atakayepewa kibarua pale Old Trafford, pindi atakapoondoshwa mtoto wa nyumbani Ole Gunner Solskjaer.

 

Rodgers aliwahi kufundisha Liverpool ambayo aliifikisha nafasi ya 2 kwenye msimu wa 2013/14. Muda mfupi baada alijiunga na Celtic kabla ya 2019 kurejea kwenye EPL na kuichukua Leicester City ambayo bado yupo nayo, mpaka sasa na wanafanya vyema ndani ya EPL.

 

Kinachoongeza matumaini kwa uwezekano wa kocha huyu kutua Old Trafford ni uwepo wa kipengele cha kimkataba ambacho, Brendan anaruhusiwa kujiunga na timu yeyote ambayo inacheza Ligi ya Mabingwa (kama timu hiyo itamuhitaji).

 

Bodi ya wakurugenzi wa United bado hawajatoa tamko rasmi kuhusu hatma ya Ole Gunnar Solskjaer lakini, kuna uwezekano kocha huyo akatimuliwa klabuni hapo muda wowote ndani ya msimu huu, pindi atakapokosa muendelezo wa matokeo ya kuridhisha.