>

PABLO AANZA KAZI SIMBA

PABLO Franco, raia wa Hispania ambaye ni kocha mpya wa Simba, leo Novemba 12 emeanza rasmi kufundisha wachezaji wa Simba.

Kocha huyo ambaye amechukua mikoba ya Didier Gomes raia wa Ufaransa ambaye alibwaga manyanga Oktoba 26 amesaini dili la miaka miwili kuwa ndani ya kikosi hicho.

Katika mazoezi ambayo yamefanyika Uwanja wa Boko Veteran alikuwa na wasaidizi wake wawili ambao aliwakuta wakiwa ndani ya Simba.

Ni Seleman Matola na Hitimana Thiery ambao hawa wapo kwenye benchi la ufundi wa Simba ambao ni mabingwa watetezi.

Kwa sasa ni maandalizi kuelekea mechi za ligi kuu ambapo mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Novemba 19.

Alionekana akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wote huku wachezaji wakiwa wenye furaha kwenye mazoezi hayo ambayo yalikuwa yakifanyika.