Home Sports NENO LA PABLO KUHUSU MCHEZO WA TAIFA STARS V DR CONGO

NENO LA PABLO KUHUSU MCHEZO WA TAIFA STARS V DR CONGO

PABLO Franco, Kocha Mpya wa Simba ameweka wazi kuwa mchezo uliowaachia maumivu Watanzania wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia ulikuwa ni wa viwango vikubwa.

Novemba 11, jana Uwanja wa Mkapa, Stars ilishuhudia Uwanja wa Mkapa ukisoma Tanzania 0-3 DR Congo ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa na umewatoa kwenye reli Stars.

Katika mchezo huo moja ya wale ambao walishuhudia mchezo huo ni pamoja na Pablo aliyeshuhudia namna likipigwa soka na kipa namba moja wa Tanzania, Aishi Manula ambaye alikuwa langoni kuokota mabao matatu kwenye nyavu zake.

Kuhusu mchezo Pablo amesema:”Ulikuwa ni mchezo mzuri tumeona kwamba kila mmoja ameona kile ambacho kimetokea lakini siwezi kuzungumza jambo lolote kuhusu wachezaji.

“Mimi nipo Simba hivyo nitazungumza mengi kuhusu Simba, asante,”.

Previous articleWASHINDI WA MKWANJA WA JACKPOT WAVUNA MINOTI
Next articleMANCHESTER UNITED KOCHA HUYU ATAJWA