XAVI Hernandez kwa sasa ni kocha mpya wa kikosi cha Barcelona na mtihani wake wa kwanza unatarajiwa kuwa dhidi ya Espanyol kwenye Barcelona Dabi itakayochezwa Camp Nou.
Dili lake ni mpaka mwaka 2024 Juni 30 ambapo ana kibarua cha kurejesha makali kwenye timu hiyo inayofuatiliwa na watu wengi duniani.
Xavi ni mkongwe wa Klabu ya Barcelona alikuwa akiinoa Klabu ya Al Sadd ya Qatar ambao wamekubali kocha huyo kuondoka hapo na ametua hapo kuchukua mikoba ya Ronald Koeman aliyechimbishwa hivi karibuni.
Alikuwa ni mchezaji hapo Barcelona kwa muda wa miaka 17 nafasi yake ni kiungo ambapo alicheza jumla ya mechi 767 alishinda mataji 25 nane yakiwa ni ya UEFA.