>

YANGA YAELEKEA ZANZIBAR, KUCHEZA LEO

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo wameanza safari kuelekeza Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Kikiwa na msafara wake chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Novemba 9 kinatarajiwa pia kuwa na kazi ya kufanya kwa kucheza mchezo wa kirafiki.

Kwenye msafara huo wamekosekana nyota wao ambao wameitwa kwenye timu zao za taifa ikiwa ni pamoja na kinara wa utupiaji ndani ya kikosi hicho, Feisal Salum mwenye mabao matatu na pasi moja ya bao.

Leo usiku Yanga itacheza na Mlandege kwenye Uwanja wa Amani saa 20:15 usiku ikiwa ni mchezo wa kirafiki.