Home Sports MAKOCHA SIMBA WASHTUSHWA NA UJIO WA PABLO

MAKOCHA SIMBA WASHTUSHWA NA UJIO WA PABLO

UJIO wa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco raia wa Hispania ambaye amepewa dili la miaka miwili umewashtua makocha waliokuwa kwenye timu hiyo kwa kuwa walikuwa hawafahamu lolote kuhusu kuwasili kwake Bongo.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa makocha hao ilieleza kuwa Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi pamoja na Hitimana Thiery ambaye alikuwa ni Kaimu Kocha Mkuu wa Simba walikuwa hawajajui kuhusu Pablo.

“Makocha wameshtuka na ujio wa Pablo kwa kuwa hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba anaweza kuja kwa ajili ya kupokea mikoba ya Didier Gomes hivyo ni kama imekuwa ni jambo la kushtukiza.

“Kikubwa ambacho walikuwa wanajua ni kwamba atakuja kocha atakuja ila kujua kwamba ni siku gani na anatokea nchi gani hapo ilikuwa ni shida kwao,” ilieleza taarifa hiyo.

Alipotafutwa Matola ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema kuwa hawezi kuzungumza alipotafutwaMwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu hakuweza kupatikana.

Previous articleYANGA YAELEKEA ZANZIBAR, KUCHEZA LEO
Next articleYANGA HAWAJUI KAMA DIARRA ATABAKI HAPO