Home Sports YANGA WASEPA NA TUZO KAMA ZOTE

YANGA WASEPA NA TUZO KAMA ZOTE

SHIRIKISHO la Soka Tanzania limebainisha kuwa sababu kubwaya kutoa tuzo kwa wale wanaofanya vizuri ni kuongeza morali kwa wachezaji, makocha pamoja na mameneja ili wafanya kazi yao kwa uzuri zaidi.

Kwa sasa tayari ligi imeanza ikiwa ni msimu wa 2021/22 na ni Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi Oktoba akiwashinda Francis Baraza wa Kagera Sugar na Mbwana Makata wa Dodoma Jiji.

Pia nyota Feisal Salum yeye alishinda tuzo ya mchezaji bora akiwashinda Ramadhan Chombo wa Biashara United na Fiston Mayele wa Yanga.

Pia Vitalis Mayanga mshambuliaji wa Polisi Tanzania amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba katika Tuzo za Shirikisho la Soka la miguu Tanzania, (TFF) kwa ligi ya NBC.

Mayanga aliwashinda wenzake wawili alioingia nao fainali ambao ni Obrey Chirwa wa Namungo na Cleophance Mkandala wa Dodoma Jiji.

Pia kocha bora kwa mwezi Septemba ni Malale Hamsini ambaye ni Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania.Malela alisepa na tuzo hiyo baada ya kuwashinda Hemed Morocco wa Namungo na Hararimana Haruna wa Mbeya Kwanza.

Previous articleSIMULIZI YA MWANAMKE ALIYEKUWA AKITESWA NA TATIZO LA HARU
Next articleMTIHANI WA KWANZA WA XAVI NI DABI