Home International LIVERPOOL YAMPA KOCHA WAKE HASIRA

LIVERPOOL YAMPA KOCHA WAKE HASIRA

KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amegeuka mbogo kwa wachezaji wake kwa kuwaeleza kuwa walicheza chini ya kiwango kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England na kuwafanya watoshane nguvu na wapinzani wao Brighton.

 

Ilikuwa ni Oktoba 30 ambapo Liverpool walikuwa wanapewa nafasi ya kushinda kwa kuwa walikuwa wametoka kuwanyoosha mabao matano Manchester United ila mambo yakawa tofauti jambo lililomkasirisha Klopp.

Kwenye mchezo huo ni Jordan Henderson dakika ya 4 alicheka na nyavu na bao la pili kwa Liverpool lilipachikwa na Sadio Mane raia wa Senegal ilikuwa dakika ya 24 na kuwafanya wawe mbele mpaka muda wa mapumziko kwa mabao 2-1.

Wageni wao wakiwa Uwanja wa Anfield ambao walikuwa ni Brighton walianza kuchomoa nyaya kupitia kwa Enock Mwepu dakika ya 41 na lile la kugawana pointi mojamoja lilipachikwa na Leandro Trossard ilikuwa dakika ya 65.

Matokeo hayo yamempa makasiriko Klopp ambapo anaamini kwamba wachezaji wake walionyesha kiwango kibovu jambo lililowapa nafasi wapinzani wao kuwafunga mabao hayo ambayo hawakustahili kufungwa.

“Tulifungua sana milango baada ya kuwa mbele ndiyo malipo yetu,kuna muda tulikuwa vizuri lakini hatukucheza vizuri,’ amesema.

Previous articleMSIMAMO WA LIGI KUU BARA HUU HAPA
Next articleSPORTPESA NGUZO YA MWENDO WA WAKONGWE YANGA