NDANI ya miaka minne tu, kampuni maarufu zaidi nchini ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa ndio inayoshikilia rekodi ya kuwa kampuni iliyoweka fedha nyingi zaidi za udhamini katika klabu kongwe zaidi nchini ya Yanga na ndio mabingwa wa kihistoria.
Yanga ndio klabu kongwe na ambayo imechukua makombe mengi zaidi ya Ligi Kuu Bara ikifuatiwa na watani wake wa jadi Simba ambao walitokea ubavuni mwa klabu hiyo kongwe zaidi. Sifa namba moja ya mashabiki wa Yanga ni wale walio na mapenzi ya dhati na klabu yao katika vipindi vyote kwa maana ya raha na shida na wamekuwa wakionyesha mapenzi ya kiwango cha juu sana kuhakikisha Yanga inafanya vema kwa kuiunga mkono. Mashabiki wa Yanga, wengi wanatambua mchango mkubwa wa SportPesa licha ya kwamba Yanga haijawa na vipindi vizuri sana lakini tayari mambo yameanza kubadilika. Wakati SportPesa inatimiza miaka minne ya kuzaliwa hapa nchini, tayari udhamini wake wa miaka minne wa kumwaga kitita cha zaidi ya Sh. bilioni moja kwa kila mwaka, ndio unaoshikilia rekodi ya kuwa udhamini mkubwa zaidi katika historia ya Yanga. Wadhamini kadhaa wamepita Yanga wakiidhamini timu ambao mchango wao unaendelea kuthaminiwa kwa kuwa umechangia kuifikisha ilipo lakini heshima kubwa ya SportPesa kuipa Yanga udhamini mkubwa zaidi ndio imekuwa gumzo zaidi. Kikosi cha Yanga kinahitaji mishahara bora, kambi bora na mengine mengi ambayo yataifanya Yanga kuwa katika mwendelezo bora wa kukiimarisha kikosi chake na unaona kadiri siku zinavyosonga mbele, Yanga wameendelea kuimarisha kikosi chao wakishirikiana na wadhamini wao wakuu SportPesa na wengine kama GSM. Mpira ni fedha na mipango ya muda mrefu na mfupi, hata ukiwa na mipango na hauna fedha, itakuwa kazi bure. Kupitia udhamini wa SportPesa imeendelea kufukuzana na watani wake wa jadi Simba kwa karibu kila msimu. Mara ya mwisho Yanga ilichukua ubingwa ni msimu wa 2016/17 ikifukuzana na mtani wake Simba baada ya kulingana pointi lakini baada ya hapo, watani wake walitawala kwa misimu minne mfululizo na katika misimu hiyo mitatu, Yanga imeendelea kubaki katika nafasi ya pili kuonyesha bado ni timu imara na mshindani sahihi wa Simba. Kubaki nafasi ya pili kwa msimu yote mitatu, hauwezi kusema Yanga imepotea kwa kuwa ndio wapinzani wakuu wa Simba katika kuusaka ubingwa wa Tanzania Bara. Ushindani umezidi kupanda lakini udhamini mkubwa kutoka SportPesa unaifanya Yanga kuzidi kuwa imara kuendelea kuupambania ubingwa na dalili zinaonyesha hivi karibuni mambo yatabadilika. Wachezaji wanahitaji huduma nzuri, wanahitaji malipo bora ili kufanya vema na udhamini wa SportPesa unaifanya Yanga kuendelea kuwa mshindani ambayo siku chache zijazo ataanza kuwa mshindi na ikiwezekana mfululizo. SportPesa imekuwa karibu na Yanga na ikifanya kazi zake kwa weledi mkubwa kama mdhamini, ndio maana haujawahi kusikia malalamiko ya fedha za udhamini kucheleweshwa lakini hujawahi kusikia malalamiko ya kuchelewa kwa mishahara au huduma bora kwa wachezaji wakiushutumu uongozi kwa kuwa tayari nao unapata uhakika kutokana na udhamini bora kutoka kwa mdhamini mkuu SportPesa anayeshirikiana na wadhamini wengine. Kabla ya udhamini wa SportPesa, Yanga zaidi ilitegemea wafadhili na si wadhamini. Kwa sasa, Yanga ina nguvu yake na mwendo bora kwa kuwa ina uhakika wa mdhamini mkuu bora ambaye anaweza kuifanya kupita katika njia sahihi inayohitaji kupita kufikia malengo yake. Mambo mengine ni hatua lakini uzoefu mkubwa wa udhamini katika mchezo wa soka wa SportPesa, umekuwa mchango mkubwa kwa Yanga. Kama unakumbuka SportPesa imewahi kuidhamini Hull City ya England ikiwa katika Ligi Kuu England lakini baadaye Everton FC ikiwa katika ligi hiyo kubwa na maarufu duniani. Uwezo wa kudhamini timu kubwa na maarufu au ligi kubwa kama ile ya Hispania, La Liga, tayari ni sababu ya uhakika kuifanya Yanga iendelee kujiamini na sasa kuendelea na mipango yake bora kuendelea kuimarisha kikosi chao ambacho bila shaka, hivi karibuni kitakuwa gumzo zaidi. Kwa kuwa kwa ushirikiano bora kabisa kutoka kwa SportPesa, Yanga inaendelea kufanya mabadiliko na kujiimarisha, mwendo unaonyesha udhamini wa miaka minne wa SportPesa umekuwa ni msaada mkubwa wa Jangwani na hivi karibuni kikosi hicho kitasimama imara na kuanza kubeba makombe mfululizo. Tayari Yanga imebeba kombe la Mapinduzipamoja na Ngao ya Jamii kwa msimu katika mechi ya fainali ambayo iliwafunga watani wake wa jadi Simba. Dalili tosha kwamba kikosi hicho kitakapoendelea kujiimarisha, kitarejea na kuanza kubeba mataji tena kwa kuwa katika Ligi Kuu Bara, mar azote kimeendelea kubaki katika nafasi ya pili.
Udhamini bora ni chachu ya maendeleo ya klabu, udhamini wa SportPesa umeendelea kuwa chachu ya kikosi cha Yanga kwenda katika mabadiliko ambayo yataifanya kuwa bora maradufu kwa kuwa iko katika mikono salama ya wadhamini na si wafadhili.
|
|
Official Website