BRENDAN HAFIKIRII KUIFUNDISHA MANCHESTER UNITED

BOSI wa Leicester City, Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hafikirii kwenda kuifundisha Manchester United.

Rodgers amesisitiza kuwa malengo yake ni kuweza kuona timu yake ya sasa inatwaa mataji zaidi.

Kocha huyo amekuwa akitajwa kwenda kuinoa Manchester United ambayo inaweza kumtimua Ole Gunnar Solkjaer.

Bosi huyo amesema:”Malengo yangu siku zote ni kuona Leicester inaendelea kuwa bora,kutwaa mataji na kuwa kwenye mwendo mzuri,”.