Home Sports KUMBE ILIKUWA NI GHAFLA TU KUMFUTA KAZI NUNO

KUMBE ILIKUWA NI GHAFLA TU KUMFUTA KAZI NUNO

IMERIPOTIWA kuwa ilikuwa ni ghafla kwa mabosi wa Klabu ya Tootenham kumfuta kazi kocha wao Nuno Espirito ambaye ametangazwa kuwa kwa sasa hatakuwa kwenye majukumu yake ya kazi.

Ikumbukwe kwamba Nuno alipokea mikoba ya Jose Mourinho ambbaye alifutwa kazi hapo Aprili 19,2021 kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo.

Nuno alichaguliwa kuwa kocha Juni 30,2021 na kuanza kufanya kazi yake kwa furaha kwa mabosi hao wanaoshiriki Ligi Kuu England.

Alianza vizuri kwa kuwa Septemba kwake anakumbuka kwamba alishinda tuzo ya kocha wa mwezi jambo ambalo liliwapa imani mashabiki na viongozi wa timu hiyo.

Mambo yaligeuka kuwa magumu ndani ya Septemba ambapo alipoteza Crystal Palace akapoteza mbele ya Chelsea na hata Arsenal pia walimnyoosha kisha mchezo wake wa mwisho ilikuwa mbele ya Manchester United aliposhuhudia vijana wake wakifungwa mabao matatu kwa nunge.

Rasmi Novemba Mosi Tottenham wamethibitisha kumfuta kazi kocha huyo huku jina la Antonio Conte likitajwa kuwa mezani kwa mabosi wa timu hiyo ambapo inaelezwa kuwa kwa sasa ana mpango wa kwenda London ili kuweza kujadili ishu ya kumpa kazi.

Previous articleBRENDAN HAFIKIRII KUIFUNDISHA MANCHESTER UNITED
Next articleORODHA YA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA