>

ARSENAL GARI IMEWAKA HUKO

AARON Ramsdale kipa wa Arsenal aliweza kuwa imara akiwa langoni wakati timu yake iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Leicester City uliochezwa Uwanja wa King Power.

Ilikuwa ni mabao ya Gabriel Magalhaes ilikuwa dakika ya 5 na lile la pili lilipachikwa na Emule Smith Rowe dakika ya 18 na kuipa pointi tatu timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta.

Arsenal inaonekana gari limewaka kwa kuwa mara ya mwishi kufungwa ilikuwa ni Agosti 28 mwaka huu baada ya hapo kwenye mechi nne haijapoteza kabisa.

Ramsadale aliweza kuokoa michomo tisa langoni mwake na hakufungwa jambo ambalo limemfanya awe gumzo kutokana na kazi yake kuitimiza vizuri.

Sasa Arsenal inafikisha pointi 17 ikiwa nafasi ya 6 huku Leicester City ikiwa nafasi ya 10 na pointi 14 zote zimecheza mechi 10.you