Home Sports KOCHA NABI ATAJWA KUIBUKIA SIMBA

KOCHA NABI ATAJWA KUIBUKIA SIMBA

IMEELEZWA kuwa, licha ya Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, kuachia nafasi ya Uenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya klabu 
hiyo, lakini bado anahusika kwenye baadhi ya mambo ikiwemo kipindi hiki cha
mchakato wa kusaka kocha 
mpya wa kuinoa timu hiyo.

 

Wakati Simba ikiwa kwenye mchakato wa kumsaka mrithi wa Kocha Didier Gomes aliyeachia ngazi Jumanne ya wiki hii, baadhi ya viongozi wa Simba wameonekana kulijadili jina la Kocha wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi.


Kwa mujibu wa chanzo 
kutoka Simba, viongozi wa timu hiyo wamekuwa bize kwenye vikao juu ya kuangalia nani
atakuwa kocha sahihi wa kurithi 
mikoba ya Gomes.

 

Mtoa taarifa huyo alieleza kwamba, katika mjadala wa kumpata mrithi wa Gomes, wapo waliolitaja jina la Nabi kutokana na kuhitaji kocha ambaye anayajua mazingira ya soka la Tanzania, lakini pia mwenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.


“Ndugu yangu suala la kupata 
kocha mpya limechukuliwa sura tofauti sana na Mo, kwani aliomba kupewa mapendekezo ya kocha anayestahili, wengi walimtaja Nabi ambaye anaonekana ufundishaji wake unaendana na matakwa yetu.

“Mazungumzo baina ya viongozi na Nabi yanaweza kufanyika muda wowote kuanzia sasa, shida wanaangalia
namna gani ataweza kuachana 
na timu yake ya sasa, lakini kama mambo yataenda vizuri, basi atachukua mikoba ya
Gomes,” kilisema chanzo hicho.

 

Spoti Xtra lilimtafuta Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said ili kuzungumzia kama wamezipata taarifa za kocha wao kutakiwa upande wa pili na kama wapo tayari
kumuachia endapo ishu hiyo 
ikiwa kweli.


Alipopatikana, Injinia Hersi 
alisema: “Hakuna taarifa kama hiyo kwetu ingawa naamini wazi kabisa hakuna kocha
anayeweza kukaa sehemu moja 
milele.


“Ila kwa taarifa hii, sidhani 
kama inawezekana mtu yoyote kumchukua kocha wetu hasa wakati huu ambao timu ina malengo makubwa ya kufika mbali. Sitaki kuonekana nabisha ila ukweli ni kwamba haiwezekani Nabi kwenda Simba kwa sasa.”

Previous articleHITIMANA AUTAKA UBINGWA SIMBA
Next articleARSENAL GARI IMEWAKA HUKO