HITIMANA AUTAKA UBINGWA SIMBA

HITIMANA Thiery, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba amebainisha kuwa timu hiyo inahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa ni timu kubwa na inawezekana kutokana na ukubwa wa timu hiyo.

Mchezo wa kwanza kukaa kwenye benchi akiwa ni kaimu baada ya Didier Gomes kubwaga manyanga ilikuwa ni mbele ya Polisi Tanzania na Simba ilishinda kwa bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.

Leo inatarajiwa kumenyana na Coastal Union kwenye mchezo wa ligi ambao nao utachezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Kocha huyo amesema:”Malengo makubwa ni kuona kwamba timu inaweza kutwaa ubingwa na inawezekana ikiwa kila mchezaji atatimiza majukumu yake.

“Ushindani ni mkubwa nasi pia tunafanya jitihada kuona kwamba timu inapata matokeo hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani kila kitu kinawezekana,”.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ipo nafasi ya tano ina pointi 7 baada ya kucheza mechi tatu kinara ni Yanga mwenye pointi 12 baada ya kucheza mechi nne.