Home Sports HUKUMU YA MORRISON NA CAS KUTOLEWA

HUKUMU YA MORRISON NA CAS KUTOLEWA

TAREHE ambayo hukumu ya kesi kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Bernard Morrison ilikuwa imepangwa, imesogezwa tena mbele hivyo inatarajiwa kutolewa Novemba 23, mwaka huu.

Wakili wa Yanga, Alex Mgongolwa ametoa ufafanuzi kuwa hukumu hiyo itatolewa siku yoyote kuanzia sasa mpaka Novemba 23, kwa mujibu wa taarifa waliyopewa na CAS.

 

Mahakama hiyo ya Usuluhishi wa michezo imetoa maamuzi hayo kutokana na upande wa mawakili wa Bernard Morrison kutuma barua ya kielektroniki (E-mail) huko CAS, ambapo walitoa pendekezo kesi hiyo itolewe hukumu kwa kuwa imekua ikiahirishwa mara kwa mara.

Awali CAS ilisema itatoa hukumu ya shauri hilo Oktoba 26, lakini haikutoka na itatoka wakati wowote kutoka sasa mpaka Novemba 23.

 

Ishu yake ni kuhusu mkataba wake ambapo Yanga wanadai kwamba mchezaji huyo alikuwa na kandarasi la miaka miwili huku mchezaji akieleza kuwa mkataba wake ulikuwa umekwisha.

 

Previous articleKOCHA YANGA AOMBA KAZI SIMBA … SOMA HAPA
Next articleNABI AWAPA MAAGIZO WACHEZAJI WAKE