Home International RONALDO :KUKOSOLEWA NI SEHEMU YA KAZI

RONALDO :KUKOSOLEWA NI SEHEMU YA KAZI

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amebainisha kwamba kukosolewa ni sehemu ya kazi jambo ambalo yeye hana mashaka nalo katika maisha yake ya kila siku.

Nyota huyo amewapuuza wale ambao wamekuwa wakimkosoa kwa kudai kuwa amekuwa akilala vizuri licha ya mwendo mbovu wa matokea wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Ronaldo aliiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool na alishuhudia Uwanja wa Old Trafford ukisoma United 0-5 Liverpool  ilikuwa ni Oktoba 24 na timu hiyo imecheza mechi nne mfululizo bila ya kuwa na matokeo mazuri.

Raia huyo wa Ureno mzee wa rekodi amesema:”Nalala vizuri usiku, nakwenda kitandani kwangu nikiwa safi kifikira kwa sababu ninajua kwamba nitaikata miezi na kushinda vitu.

“Kukosea siku zote ni sehemu ya kazi sihofii juu ya hilo na kiukweli naona ni jambo zuri. Kama wana hofu na mimi ama wanazungumza kuhusu mimi kwa sababu wanajua uwezo wangu na thamani yangu, siku bado ipo  Kwa hiyo ni vizuri,”.

Previous articleYANGA YAIPIGIA HESABU AZAM FC
Next articleSIMBA MATUMAINI MAKUBWA NDANI YA LIGI KUU BARA