Home Sports BOCCO AWEKA REKODI,KIBU MAJANGA MATUPU

BOCCO AWEKA REKODI,KIBU MAJANGA MATUPU

 

WAKIWA kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Mkapa, nyota wawili wa Simba waliweka rekodi zao za kipekee.

 

Ni nahodha John Bocco ambaye ni mchezaji bora wa msimu wa 2020/21 na mshikaji wake Kibu Dennis katika suala la kucheka na nyavu kila mmoja alifanya jambo lake huku Bocco akiweka rekodi tamu na Kibu kwake ikiwa ni majanga matupu.

 

Picha nzima ilikuwa Uwanja wa Boko Veteran juzi kwenye mazoezi ambapo Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes aliwataka washambuliaji hao kufunga bao kwa pigo moja baada ya kupokea pasi wakiwa ndani ya 18.

 

Bocco alipopata mpira akiwa ndani ya 18 alianza kumtungua Beno Kakolanya kwa bao la kichwa kisha mpira wake mwingine alioupata alimtungua Jeremia Kisubi na Ally Salim na kuandika rekodi ya kuwatungua makipa watatu wa timu hiyo ndani ya 18.

 

Kibu kwake ilikuwa majanga kwa kuwa mashuti matatu aliyopiga baada ya kupokea mpira alikwama kuyazamisha nyavuni kwa kupaisha mawili na moja lilidakwa na shuti lake la nne lililitemwa na Kisubi kisha Gomes akamruhusu afunge ndipo akafanikiwa kulijaza kimiani.

Kuhusu mchezo wa leo Kocha Msaidizi wa Simba, Hitimana Thiery alisema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wanahitaji kupata ushindi ili kutinga hatua ya makundi.

“Tunahitaji kutinga hatua ya makundi na ili iwe hivyo ni lazima tuweze kushinda, kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi kwanza kisha baada ya hapo tutatoa burudani,”.

Previous articleSALAH AGOMA KUSEPA LIVERPOOL
Next articlePACHA YA BANGALA,JOB NA DJUMA YAJIBU YANGA