
SAKHO,BANDA WAMPA KIBURI PABLO KIMATAIFA
KUREJEA kwa Pape Ousmane Sakho ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya ASEC Mimosas na kuimarika kwa kiwango cha winga Peter Banda, kumempa kiburi Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco kufanya vizuri katika mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Union Sportive Gendarmerie Nationale ya nchini Niger. Simba leo Jumapili wanatarajiwa kumenyana na Union Sportive Gendarmerie Nationale katika mchezo wa pili wa Kundi D ndani ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa kwenye Dimba la Général Seyni…