MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Alhamisi, mtaani nakala yake ni 500.
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Alhamisi, mtaani nakala yake ni 500.
KATIKA michezo wa kwanza leo Yanga wameweza kuibuka na ushindj wa mabao 2-0 mbele ya Taifa Jang’ombe. Mabao ya Yanga yametupiwa na Heritier Makambo dakika ya 32 na lile la pili limepachikwa na Dennis Nkane. Ni bao la kwanza kwa Nkane baada ya kuibuka hapo akitokea kikosi cha Biashara United na amefunga bao hilo dakika…
MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi Yanga wanakwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja kwa nunge. Dakika 45 zimekamilika na ubao unasoma Yanga 1-0 Taifa Jang’ombe. Bao la kuongoza limefungwa na Heritier Makambo dakika ya ya 32 akiwa nje ya 18. Pia nyota mpya wa Yanga Dennis Nkane ameanza kikosi cha kwanza leo Januari 5,2022…
SELEMAN Matola kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa ushindi ambao wameupata leo ni furaha kwao na pongezi kwa wachezaji. Ushindi wa mabao 2-0 dhidi Selem View ambao walikwama kupiga shuti ambalo limelenga lango mbele ya Simba. Ni mabao ya Pape Sakho dakika ya 24 na liliweza kudumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza. Kipindi…
UWANJA wa Amaan kwa sasa ni mapumziko mchezo wa Kombe la Mapinduzi na timu zote zimeyeyusha dakika 45. Ubao unasoma Simba 1-0 Selem View na mashabiki wengi wamejitokeza kushuhudia mchezo huu. Ni bao la Pape Sakho aliyepachika bao hilo dakika ya 24 na kuifanya Simba kuwa mbele kwa bao hilo. Leo langoni kwa Simba ni…
AHMED Ally, Ofisa Habari wa Simba ameweka wazi kuwa malengo yake makubwa ni kuweza kuona timu hiyo inaweza kufanya vizuri zaidi kwenye ulimwengu wa mitandao ya kijamii licha ya kwamba kwa sasa inafanya vizuri zaidi pamoja na kuweza kuwazungumzia kwa ukaribu wachezaji wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na Aishi Manula, Pape Sakho na Kibu…
KLABU ya Yanga leo Januari 5 imeingia makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Cards kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa timu hiyo. Hiyo ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji ambapo kadi moja itauzwa shilingi 29,000. Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema kuwa…
PAMOJA na kuwepo na tetesi nyingi za kuachwa pale Yanga, kipa chaguo la pili Ramadhani Kabwili, amevunja ukimya kwa kusema yeye bado ni mali ya Wanajangwani hao na kwamba ameomba tu mapumziko kwa muda kisha atarudi kukiwasha kikosini hapo. Kabwili aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2016/17 akiwa kinda kabla ya kupandishwa kikosi cha…
MASTAA wa Yanga, Khalidi Aucho na Fiston Mayele, hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe na kwamba wataunguruma dhidi ya KMKM kesho kutwa Ijumaa. Aucho ameshindwa kusafiri na kikosi hicho kufuatia kuomba ruhusa ya kwenda kwao Uganda kwa ajili ya kuiona familia yake, huku Fiston Mayele naye yupo…
KUELEKEA mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi kesho Jumanne, uongozi wa Simba umetamba kuwa kikosi chao kiko tayari kwa ajili ya mashindano hayo na malengo yao makubwa ni kuwavua ubingwa watani zao wa jadi Yanga. Michuano ya Kombe la Mapinduzi ilianza rasmi jana Jumapili kwa mchezo mmoja kati ya Namungo dhidi…
UONGOZI wa klabu ya Yanga, leo Januari 05, 2022, wamezungumza na wanahabari kuhusiana na uamuzi wao wa kuunganisha wanawachama na klabu yao kidigitali.
IBRAHIM Ajibu kiungo mpya wa Azam FC ambaye amesaini dili la mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo akitokea Klabu ya Simba ameweka wazi sababu za kuondoka Simba.
Ni utamaduni, mwezi Januari huwa na michezo mingi. 2022 ni muendelezo wa burudani kwenye ulimwengu wa soka. Nusu fainali ya Carabao, muendelezo wa Bundesliga na SerieA kuchezwa wiki hii. Pamba mkeka wako kwa Odds hizi; Jumatano hii, Chelsea watarejea uwanjani kuwakabili Tottenham Hot Spurs. The Blues wanaingia uwanjani kuikabili Spurs ambapo hii ni London…
KIUNGO mpya wa Azam FC Ibrahim Ajibu ameanza kazi na uzi huo katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi na alishuhudia timu hiyo ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Meli 4 City. Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilishuhudia bao moja pekee lililofungwa na Chilunda dakika ya 13 na lilidumu mpaka dakika ya 45….
MOJA ya sehemu ambayo hukusanya mashabiki wengi wa mpira ni Viwanja vya Bunju Complex ambapo Simba SC na Simba Queens hufanyia mazoezi. Usafiri mkubwa kwa mashabiki ni bodaboda na wakati wa mazoezi mashabiki hupanda mpaka juu ya bajaji kutazama maujuzi ya wachezaji.
CRISPIN Ngushi, aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza sasa rasmi ni mali ya Yanga. Nyota huyo ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia jumla ya mabao matatu na alikuwa ni kinara ndani ya Mbeya Kwanza. Alikuwa ni mshambuliaji wa kwanza msimu wa 2021/22 kufunga bao la kideo ambalo ni Acrobatic ilikuwa mbele ya Mbeya City katika mchezo…