BREAKING:AZAM FC YAACHANA NA MAKOCHA WAO

UONGOZI wa Azam FC umefikia makubaliano ya kuachana na makocha wao wawili kwenye majukumu ya kuinoa timu hiyo hivyo watabadilishiwa majukumu. Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeeleza namna hii:”Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia. “Hata hivyo, makocha…

Read More

SIMBA YACHEKELEA USHINDI

SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa ushindi ambao wameupata mbele ya Asante Kotoko walistahili na kama wagekuwa makini zaidi wangeshinda kwa mabao mengi. Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Zoran Maki imealikwa kwenye mashindano maalumu nchini Sudan ambayo yameandaliwa na Klabu ya Al Hilal. Mchezo wao wa kwanza Simba ilishinda mabao 4-2 huku…

Read More

NABI:HAITAKUWA KAZI RAHISI KUTWAA UBINGWA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa jambo ambalo linawafanya wazidi kujipanga kwa mechi zao. Yanga ni mabingwa watetezi wa taji la ligi ambalo walitwaa msimu wa 2021/22 kutoka mikononi mwa watani zao wa jadi Simba. Timu hiyo imecheza mechi mbili na kukusanya pointi sita, ilishinda mabao 2-1…

Read More

KOCHA LIVERPOOL ABADILI MAAMUZI

KLABU ya Liverpool imeweka dau la pauni milioni 60 kuinasa saini ya kiungo wa Barcelona, Frenkie de Jong. Mpango wa timu hiyo ni kuinasa saini ya nyota huyo ili aweze kutua ndani ya Anfield kwa ajili ya kucheza mechi za Ligi Kuu England pamoja na mashindano mengine. Jurgen Klopp Kocha Mkuu wa Liverpool amebadili mawazo…

Read More

SIMBA YAANZA KWA USHINDI UGENINI KIMATAIFA

 MCHEZO wa kwanza wa kirafiki nchini Sudan kwenye mashindano maalumu ambayo Simba kutoka Tanzania imealikwa na Al Hilal wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 Asante Kotoko. Kipa namba moja kwenye mchezo huo alikuwa Ally Salim ambaye alibeba mikoba ya Aishi Manula na Beno Kakolanya ambao wapo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa…

Read More

TAIFA STARS YAPOTEZA MBELE YA UGANDA

TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kuwania kufuzu CHAN. Dakika 45 za mwanzo timu zote zilikwenda vyumba vya kubadilishia nguvo wakiwa hawajafungana baada ya kutoshana nguvu. Zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kukamilika, Uganda waliweza kupachika bao kupitia kwa Travis Mutyaba dakika ya 87…

Read More

LIVERPOOL WANASIFA KWELI WACHAPA 9-0

IKIWA Uwanja wa Anfield, Klabu ya Liverpool imeibuka na ushindi mkubwa wa mabao 9-0 dhidi ya Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Huu unakuwa ni ushindi mkubwa ndani ya Ligi Kuu England ambayo imeanza kwa kasi na wa kwanza kwa Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp. Staa Robert Firmino ambaye anafikisha mabao 100 akiwa na…

Read More

TAIFA STARS KAZINI LEO KUIKABILI UGANDA

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo kuikabili Uganda. Huu ni mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani, (CHAN), Uwanja wa Mkapa saa 10:00. Poulsen amesema kuwa wanatambua Uganda ni moja ya timu ngumu…

Read More

ARSENAL WAPINDUA MEZA NA KUJIIMARISHA JUU

UPINDUAJI wa meza mbele ya Fulham ambao walitangulia kupachika bao dakika ya 56 kupitia kwa Aleksandar Mitrovic unawafanya Arsenal kuanza kwa kasi msimu wa 2022/23. Dakika 8 zilitosha kwa Klabu ya Arsenal inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta kufanya yao kwa kuanza kufunga mabao yao. Ni Mardtin Odegaard aliweza kuweka usawa ilikuwa dakika ya 64…

Read More