
YANGA YAIPIGIA HESABU NDEFU REAL BAMAKO
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa unahitaji kuvunja rekodi ya mabao waliyowafunga TP Mazembe kwenye mchezo wa kimataifa. Timu hiyo ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi Machi 8 in kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Real Bamako ambapo mchezo wao uliopita waligawana pointi mojamoja nchini Mali. Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema…