HESHIMA KWA MKAPA KIMATAIFA USHINDI

  HESHIMA ya Uwanja wa Mkapa kwenye mechi za kimataifa ni ushindi hilo linawastahili Watanzania na mashabiki wote ambao wanapenda matokeo mazuri.

  Ipo hivyo kwa sasa wawakilishi wetu kwenye anga la kimataifa Yanga na Simba wanakazi kubwa kusaka pointi tatu muhimu.

  Simba wataanza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo watakabiliana na Vipers mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

  Ushindi wa ugenini haina maana kwamba itakuwa rahisi kushinda hapa nyumbani kwani ni Simba wenyewe walikwama kupata ushindi dhidi ya Raja Casablanca.

  Kila kitu kipo tofauti mbinu za Raja na Vipers ni tofauti lakini muhimu kwa wachezaji kujituma kufanya kweli kusaka ushindi nymbani.

  Mashabiki wanapenda kuona ushindi kwa timu yao ili kufufua matumaini ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Yanga ni kwenye Kombe la Shirikisho na kazi yao ni dhidi ya Real Bamako hawa itakuwa Jumatano moja ya kazi kubwa na muhimu kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

  Ni dakika 90 za kazi nzito kutokana na kila timu kuhitaji pointi tatu lakini wachezaji wa Yanga wakiamua kushinda mchezo huo inawezekana kutokana na faida waliyonayo ya ushindi dhidi ya TP Mazembe.

  Kushinda mchezo dhidi ya TP Mazembe kunawapa nguvu lakini sio matokeo ni mpaka pale watakapotumia nafasi watakazopata.

  Previous articleTIZI LA MWISHO LA SIMBA LILIKUWA NOMA
  Next articleYANGA YAIPIGIA HESABU NDEFU REAL BAMAKO