Home Sports YANGA YAIPIGIA HESABU NDEFU REAL BAMAKO

YANGA YAIPIGIA HESABU NDEFU REAL BAMAKO

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa unahitaji kuvunja rekodi ya mabao waliyowafunga TP Mazembe kwenye mchezo wa kimataifa.

Timu hiyo ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi Machi 8 in kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Real Bamako ambapo mchezo wao uliopita waligawana pointi mojamoja nchini Mali.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi za kimataifa na kupata ushindi nyumbani kutaongeza nguvu ya kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali.

“Tulishinda mabao matatu dhidi ya TP Mazembe wakasema kwamba hatuwezi kufunga mabao mengi sasa kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Real Bamako tunahitaji kufunga mabao mengi zaidi.

“Uzuri ni kwamba kuna wachezaji wazuri ambao wanafanya kazi kubwa kila kitu tunaamini kwamba kitakuwa sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu,” .

Yanga ipo kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imekusanya pointi kibindoni imecheza mechi nne imeshinda mchezo mmoja, sare moja na imenyoosha mchezo mmoja.

Mchezo wake wa kwanza Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe na kuwafanya wakusanye pointi tatu wakiwa nyumbani mazima.

Previous articleHESHIMA KWA MKAPA KIMATAIFA USHINDI
Next articleKMC KWENYE KIBARUA KINGINE TENA