Home Sports KMC KWENYE KIBARUA KINGINE TENA

KMC KWENYE KIBARUA KINGINE TENA

IKIWA imefungashiwa virago kwenye Kombe la Azam Sports Federation ubao wa Uwanja wa Manungu uliposoma Mtibwa Sugar 1-0 KMC kuna kibarua kingine kizito kinawakabili.

KMC chini ya Kocha Hitimana Thiery haijawa na mwendo mzuri kwenye mechi zake za ligi na sasa matumaini ya kutwaa taji la Azam Sports Federation yameyeyuka baada ya kuondolewa hatua ya 16 bora.

Kigongo kingine kinachowakabili ni dhidi ya Kagera Sugar ambao ni mchezo wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru, Machi 9 mwaka huu.

Wakusanya mapato hao kwa sasa lile pira kodi limekuwa gumu kutokana na kushindwa kupata matokeo chanya ambapo ilitoka kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Azam FC mchezo wa ligi na Machi 4,2023 ilichapwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 14 na pointi 23 inakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya 6 na pointi zake 32.

Previous articleYANGA YAIPIGIA HESABU NDEFU REAL BAMAKO
Next articleSTAA WA MABAO YA KIDEONI AANDALIWA KUIMALIZA VIPERS