STAA WA MABAO YA KIDEONI AANDALIWA KUIMALIZA VIPERS

  MOHAMED Mussa mshambuliaji wa kikosi cha Simba ni miongoni mwa mastaa ambao wameanza mazoezi kuikabili Vipers kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Simba ina kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Vipers leo Machi 7 ikiwa ni mchezo wa nne katika kundi C kwenye mchezo uliopita ilishuhudia ubao wa Uwanja wa St Mary’s ukisoma Vipers 0-1 Simba.

  Kwenye kambi ya mazoezi ambayo Bunju chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira pamoja na yale yaliyofanywa Uwanja wa Mkapa, Machi 6 Mussa ambaye alifunga bao la kideo kwenye mchezo dhidi ya African Sports alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa mazoezini.

  Mbali na mshambuliaji huyo ambaye ni bao lake la kwanza kufunga akiwa na Simba msimu huu katika mashindano hata aliyempa pasi Moses Phiri naye yupo kwenye kikosi hicho.

  Wengine ni Jean Baleke, Henock Inonga beki pekee mwenye bao katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa, Saidi Ntibanzokiza, Shomari Kapombe, John Bocco, Erasto Nyoni, Ally Salim na Kennedy Juma ni miongoni mwa wachezaji wa Simba wanaoivutia kasi Vipers.

  Ni Kibu Dennis huyu anatarajiwa kuukosa mchezo huo kwa kuwa yupo kwenye program maalumu itakayomrejesha kwenye ubora wake baada ya kutokuwa fiti.

  Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Vipers.

  “Wachezaji wetu wapo tayari na wapo kambini wakiendelea na maandalizi kwa ajili ya kuwapelekea pumzi ya moto wapinzai wetu Vipers tunawaheshimu lakini tunahitaji pointi tatu zao hilo ni jambo la muhimu kwetu,” .

  Previous articleKMC KWENYE KIBARUA KINGINE TENA
  Next articleSABABU YA SURE BOY KUIKOSA REAL BAMAKO IPO HIVI