Home Sports SABABU YA SURE BOY KUIKOSA REAL BAMAKO IPO HIVI

SABABU YA SURE BOY KUIKOSA REAL BAMAKO IPO HIVI

VIONGOZI wa Klabu ya Yanga ikiwa ni pamoja na Rais Injnia Hersi Said leo Machi 7,2023 leo mchana walishiriki kwenye mazishi ya kumuaga mtoto wa mchezaji Salum Abubakar, Magomeni, Dar es Salaam.

Pia Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi naye alikuwa miongoni mwa waliohudhuria.

Kwa mujibu wa Nabi, kiungo huyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachopambana na Real Bamako kesho Machi 8,2023 Uwanja wa Mkapa.

Nabi ameweka wazi kuwa wachezaji wote wapo tayari na wanamuombea kheri kiungo huyo kutokana na matatizo ya kifamilia.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Previous articleSTAA WA MABAO YA KIDEONI AANDALIWA KUIMALIZA VIPERS
Next articleHIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA REAL BAMAKO